Jumamosi, 18 Agosti 2018

MAWAZO 150 YA KUFANYA BIASHARA AU KUANZISHA BIASHARA

Watu wengi wamekuwa wakiangaika hama kuwauliza watu wao wa karibu ni biashara gani afanye au ukimuuliza ni biashara gani unataka kufanya atakuambia mimi nataka kufanya biashara yoyote ili mradi tu iwe inaniingizia faidi. Kuwa maalum(specific) na usipende kufanya biashara yoyote kwani kama ujui unataka kwenda wapi basi uelekeo wowote utakupeleka usipotaka. Si mawazo yote yatakuwa sawa kwako,chagua wazo moja tu la biashara na uanze kulifanyia kazi na uanze sasa kwa kutumia chochote ulichonachoo usingoje kuwa na fedha nyingi ndiyo uanze.Chagua eneo gani upo vizuri na kuchukua hatua sasa

1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha

2.Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.

3.Kutengeneza na kuuza tofali.

4.Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.

5.Kuanzisha kituo cha redio na televisheni.

6.Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano.

7.Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k

8.Kushona na kuuza nguo.

9.Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali.

10.Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng?ombe, Kuku, Bata, na wengine.

11.Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.

12. Kutoa ushauri mbalimbali waKitaalamu.

13.Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza.

14.Kusajili namba za simu na kuuza vocha

15.Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta

16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.

17.Kuuza Mitumba.

18.Kusimamia miradi mbalimbali

19.Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali.

20.Kufungua banda la chakula na chips.

21.Kukodisha turubai viti na meza.

22.Kufungua Supermarket.

23.Kufungua Saluni.

24.Kufungua Bucha.

25.Video Shooting & Editing.

26. Kufungua Internet cafe.

27.Duka la kuuza matunda.

28.Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.

29.Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati.

30.Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT.

31.Kuchapa vitabu, bronchures, n.k32.Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor).

33.Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k.

34.Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.

35.Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.

36.Kukodisha Music

37.Kuanzisha Mradi wa Taxi

38. Kuanzisha mradi wa Daladala.

39.Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine.

40. Kununua magenerator na kukodisha

41.Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu.

42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP).

43.Kuuza mabati na vigae

44.Kujenga apartments

45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote.

46.Kufungua Duka la samaki.

47.Kufungua Duka la nafaka.

48.Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.

49.Kujenga hostel

50.Kuuza vocha na vingamuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.

51.Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi.

52.Ufundi simu

53.Kufungua Hospitali, Zahanati.

54.Maabara ya Macho, Meno

55. Kuchimba/Kuuza Madini

56.Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax.

57.Kuuza miti na mbao.

58.Kufungua Grocery, bar

59.Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha.

60.Kucharge simu/battery.

61.Duka la TV na vifaa vingine.

62.Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering).

63.Banda la kupigisha simu.

64.Kuuza na kushona Uniform za shule.

65.Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.

66.Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari

67.Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe

68.Kuuza fanicha.

69.Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi ya magari na mitambo.

70.Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)

71.Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.

72.Kuuza vioo

73.Kushona na kukodisha nguo za harusi.

74.Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari

75.Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).

76.Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)

77.Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi

78.Kufungua studio ya kutengenezavipindi vya redio na televisheni

79.Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)

80.Kufungua benki.

81.Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga.

82.Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k

83.Kuwa dalali wa vitu mbalimbali.

84.Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)

85.Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.

86.Kuanzisha viwanda mbalimbali

87.Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.

88.Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali

89.Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha

90.Kutengeneza antenna na kuuza

91.Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao

92.Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo

93.Biashara ya kuagiza magari

94.Kufanya biashara za Jukebox

95.Kukodisha matenki ya maji

96.Kufungua duka la kuuza Asali

97.Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha

98.Kufungua Duka la vinyago, batiki

99.Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZYPESA

100.Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).

101.Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.

102.Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).

103.Kufungua Kampuni ya Ulinzi

104.Kufungua kampuni ya”Clearing and fowarding”

105.Kuchezesha vikaragosi

106.Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki

107.Kuuza baiskeli

108.Kuuza magodoro

109.Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe,vijiko,

110.Kuuza marumaru (limestones)

111.Kuuza kokoto

112.Kuuza mchanga

113.Kufundisha Tuisheni

114.Biashara za bima

115.Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)

116.Biashara za kitalii

117.Biashara za meli na maboti.

118.Kampuni ya kuchimba visima

119.Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea

120.Kuuza mkaa

121.Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali

122.Kampuni ya kupima ardhi

123.Kampuni ya magazeti

124.Kuchapa (printing) magazeti

125.Kuuza magazeti

126.Kuchimba mafuta

127.Kiwanda cha kutengeneza mabati

128.Kiwanda cha kutengeneza fanicha

129.Kiwanda cha kutengeneza matairi

130.Kutengeneza vitanda vya chuma

131.Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha.

132.Kukodisha makapeti

133.Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.

134.Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.

135.Kazi ya ususi na kusafisha kucha.

136.Kuuza Gypsum

137.Malori ya kubeba mafuta na Mizigo

138.Duka la kuuza mboga za majani

39.Duka la kuuza maua.

140.Kampuni ya kuzoa takataka

141.Kampuni ya kuuza magari

142.Kuuza viwanja

143.Uvuvi

144.Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi

145.Uchoraji wa mabango.

146.Duka la kuuza silaha

147.Ukumbi wa kuonesha mpira

148.Biashara ya Multi-Level Marketing-MLM

149.Yadi kwa ajili ya kupaki magari

150.Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo..

Amua haraka nini unataka kufanya nini kwa ajili yako na maisha yako na kama kweli unataka kufanya biashara/ujasiriamali napenda kukusisitiza uanze sasa kwa kutumia chochote ulichonacho kwani ndege mmoja aliyo mkonono mwako ni bora zaidi kuliko 100 walio angani
Kwanza mtumaini Mungu utafanikiwa kuanza biashara yako ulioiwaza 0743 788 246

NJIA 9 ZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO BILA KITUMIA PESA KUBWA

Matangazo ni swala muhimu kwa kila biashara. Tatizo linatokea pale ambapo biashara inashindwa kumudu gharama za matangazo, hasa matangazo ya gharama kubwa.
Naamini wewe kama mjasiriamali unafahamu kuwa kuna wakati bajeti ya biashara inakuwa imebana. Hivyo swala la kujitangaza linakuwa na changamoto.
Fuatilia makala hii kwa karibu ili nikufahamishe njia 9 unazoweza kuzitumia kutangaza biashara yako bure au kwa gharama nafuu sana.
1. Tumia tovuti
Tovuti au blog ni njia rahisi na ya gharama nafuu ya kujitangaza. Ikiwa una blog au tovuti ambayo inaidadi nzuri ya watembeleaji, unaweza kuweka tangazo la biashara yako hapo na likaonekana kwa watu wengi zaidi.
2. Tumia mitandao ya kijamii
Kama ilivyo wenye njia ya blog, vivyo hivyo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram n.k. ili kujitangaza.
Kumbuka hivi leo karibu kila mtu anatumia mitandao ya kijamii. Hivyo kutangaza biashara yako kupitia kurasa au akaunti zako za mitandao hii ni rahisi na utawafikia watu wengi zaidi.
3. Tengeneza vifungashio au zawadi ndogo
Siyo lazima uwe na pesa nyingi ndipo utoe zawadi au huduma ya vifungashio vyenye chapa yako. Unaweza kubuni na kuchapisha vifungashio vyenye jina na maelezo mafupi kuhusu biashara yako ili kujitangaza.
Unaweza kutoa zawadi ndogo kama vile kalamu au shajara (diary) vyenye maelezo ya biashara yako.
4. Tengeneza kadi za kibiashara na vipeperushi
Unapopewa kadi ya kibiashara (business card) au kipeperushi lengo lake hasa ni kujitangaza. Unaweza kutengeneza kadi za kibiashara pamoja na vipeperushi vyenye maelezo mafupi kuhusu biashara yako.
Naamini njia hii ni nafuu sana kuliko kuweka tangazo kwenye televisheni wakati wa habari.
5. Kuwa wakala wa biashara kubwa
Kuwa wakala wa biashara kubwa ni njia moja nzuri ya kujitangaza na kuongeza wateja. Mara nyingi biashara kubwa huwatangaza mawakala wao katika matangazo yao ya gharama kubwa.
Hivyo, kwa kuwa wakala wa biashara au kampuni kubwa kama vile makampuni ya simu, bima, dawa, pembejeo, au fedha; utakuwa umepata nafasi ya kutangazwa bure kabisa.
6. Hudhuria semina na makongamano
Njia nyingine nzuri na rahisi ya kujitangaza ni kwa kuhudhuria semina, makongamano au sehemu zenye mikusanyiko.
Uwapo katika maeneo haya, hakikisha unatafuta angalau nafasi ya kutoa salamu katika maeneo haya, ukipewa nafasi ya kuzungumza taja tu hata jina la biashara yako kwani ina maana kubwa sana. Unaweza kuvaa pia mavazi yenye maelezo au matangazo ya biashara yako.
7. Jitolee au toa misaada
Naamini mara kadhaa umewahi kuona wafanyakazi wa kampuni au biashara fulani wakitoa misaada au hata kujitolea kufanya kazi kama vile usafi wa mazingira.
“Hakuna chakula cha bure kwenye uchumi.”

Je ni nini hasa msingi wa swala hili? Kama wanauchumi wa kale walivyotangulia kusema kuwa hakuna chakula cha bure kwenye uchumi, vivyo hivyo matendo ya kujitolea au msaada yana lengo fulani.
Mara nyingi makampuni au biashara fulani zinapotoa misaada waandishi wa habari hurekodi na kutangaza habari hiyo. Hii ni njia nzuri sana ya kujitangaza.
8. Endesha shindano
Nani asiyependa kushinda? Naamini hata wewe unapenda kushinda zawadi fulani.
Ili ushinde unatakiwa kununua bidhaa au kusambaza habari kuhusu biashara fulani, je kwa njia hii hujaitangaza biashara hiyo? Naamini utakuwa umefanya hivyo tayari.
Unaweza kuendesha shindano dogo lenye zawadi za kawaida kama vile mikoba, vocha za simu, vinywaji, kalamu au hata bidhaa unazouza. Kwa njia hii utajitagaza kwa gharama nafuu kabisa.
9. Toa elimu au ushauri bure
Kama kuna elimu au ushauri fulani unaoweza kuutoa ambao unaendana na biashara yako; fanya hivyo sasa.
Kwa njia hii utafahamika na kuwafikia watu wengi zaidi na hivyo kuitangaza biashara au huduma yako kwa urahisi na  kwa gharama nafuu kabisa.
Hitimisho
Kufanikiwa katika kitu chochote kunahitaji mikakati sahihi na ubunifu. Naamini umeona jinsi ambavyo unaweza kutumia njia mbalimbali kujitangaza kwa bei nafuu au bure kabisa.
Naamini hutoumiza tena kichwa kufikiri njia za kupata pesa nyingi kwa ajili ya matangazo ya gharama kubwa.
0743 788 246
@abiolasolidaritygroup@gmail.com

Alhamisi, 9 Agosti 2018

HATUA KUMI (10) ZA KUANZISHA BIASHARA NDOGO

EHEMU YA 1

Ndoto za kuanzisha  zinaweza kuwa kweli haraka na kwa urahisi zaidi endapo mtu atafuata taratibu hizi pamoja na kufanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango kamili (mchanganuo) wa biashara yake iwe ni katika karatasi ama kichwani mwake.

Chagua mfumo wa bishara kisheria

Kuchagua mfumo wa biashara yako kisheria ni uamuzi wa msingi kabisa kabla ya kuanza bishara, kwani kuja kubadili baadaye ni jambo la ghrama na usumbufu mkubwa.

Mifumo ya biashara kisheria ipo ya aina tatu;

(a)        Biashara ya mtu bianafsi.

(b)        Biashara ya ubia.

(c)        Biashara ya kampuni yenye dhima ya ukomo (Limited company)

Biashara nyingi za rejareja hasa zile ndogo ndogo wanatumia sana mfumo huu wa  biashara ya mtu mmoja au binafsi. Faida na harasa za mifumo  yote 3 imefafanuliwa kwa undani sana katika vitabu mbalimbali kikiwemo kitabu kikubwa “Jifunze Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali”

Chagua jina la biashara yako.

Unaweza ukawa na mpango mzuri sana wa biashara yako ya rejareja lakini ukaipa jina lisilofaa ukawa umeharibu kila kitu. Kuipa biashara jina ni hatua muhimu sana ingawa unaweza kuona ni kazi nyepesi tu kufanya hivyo. Ni kazi inayohitaji ufikirie kwa umakini mkubwa, unapotaka kuipa biashara yako ya rejareja jina linalofaa  zingatia vipengele hivi hapa chini;

Orodhesha  kwenye karatasi  bidhaa ama huduma unazotoa, maneno yote yanayohusiana na biashara unayotarajia kuifanya pamoja na mazingira na eneo itakapokuwa.Fanya utafiti kwa kuangalia majina ya biashara kama ya kwako zilizokuzunguka, unanweza pia ukatazama kwenye mtandao wa intanet n.k mpaka utakapopata jina utakaliona unaridhika nalo.

    Jina linapaswa liwe;

Rahisi kueleweka kimatamshi na kimaandishi.

Usichague jina lenye mlengo hasi mfano mmoja ni  café moja jamaa alitumia jina linalokashifu timu fulani ya mpira.

 Usichague jina litakalopotosha watu wala lenye maana zaidi ya moja.

 Zingatia herufi jina la biashara yako litakapoanguakia kwenye orodha kama za yellow page n.k.

 Chagua jina litakalowakilisha kile kitu hasa utakachofanya na siyo litakalominya baadhi ya shughuli zako.

 Chagua jina utakalojivunia na siyo litakalokufanya uone aibu hata kuliwakilisha mbela za watu.

Usitumie majina ya jumla yanayowakilisha vitu jumla mfano; Nafuuu store, Bei rahisi duka n.k. majina kama hayo ni vigumu kuyasajili kama alama yako ya biashara.

Baada  ya kupata jina la biashara yako,  jaribu kuuliza watu wa karibu ikiwa  nao kama watalipenda. Wakiona linafaa basi lipitishe, ukiona wengi wamelitilia mashaka unaweza  ukarudi tena kwenye orodha yako upya.

Ipe  biashara yako namba ya Utambulisho wa mlipa kodi TIN

Ni vizuri  ukaenda kuisajili biashara yako mamlaka ya mapato “TRA” tawi lililopo karibuni na wewe wakupe namba ya mlipa kodi(TIN). Hatua hii hulipi gharama yeyote, ni bure. Baada ya kujaza fomu zao wanakupa hati na  kukufungulia faili ambalo baadae ndilo huja kulitumia utakapokwenda kulipa kodi ya mapato. Ikiwa biashara yako ni ndogo sana unaweza ukaianza hivyo hivyo tu bila TIN lakini baadae ukaja kujisajili.

Uchaguzi wa  ni bidhaa gani utakazouza.       

Kwa biashara ya duka la rejareja la mtaani hakuna ukomo wa bidhaa unazotakiwa kuuza. Cha kuzingatia hapa ni kuangalia katika utafiti wako uliofanya ni bidhaa zipi unaona wakazi wa eneo husika wanapendelea zaidi kununua.

Vigezo vingine ni pamoja na faida, angalia ni bidhaa zipi zenye faida kubwa kwa mfano aina fulani ya maji yanaweza kuwa yananunuliwa kwa wingi sana lakini faida yake ni kidogo mno. Hivyo ni juu yako kuamua upate faida kidogo uuze sana au faida kubwa lakini mauzo kidogo.

Angalia pia bidha zinazoendana na wakati uliopo, ushindani: ukichagua bidhaa za kipekee unaweza ukashindana hata na biashara kubwa kubwa.

Katika vitu muhimu sana unavyopaswa kufanya kabla haujaanzisha duka lako ni kuandaa mpango kamili wa biashara, mpango unaweza kuwa upo kichwani mwako tayari lakini ni vizuri zaidi ukauandika katika karatasi hata kama  hautafuata taratibu rasmi za kuandika, unaweza tu ukaorodhesha mambo yako yote muhimu unayotarajia kuyafanya ili kukamilisha malengo ya biashara yako pamoja na gharama utakazotumia, pia faida au mauzo unayotarajia kwa siku, mwezi au mwaka, na tayari huo unatosha kuitwa mpango wa baishara yako.

Mwanamke akiuza duka la rejareja.

Ni kama vile unapotoka nyumbani kwenda sokoni kununua vitu vya nyumbani, unaorodhesha vitu vyote unavyotarajia kwenda kununua kwenye karatasi pamoja na bajeti ya fedha utakazotumia. Michanganuo ya biashara kwa undani zaidi pamoja na mifano yake hai imefafanuliwa katika kitabu  “Jifunze Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali”

Fahamu sheria na taratibu za mamlaka husika.

Watu wengi baaba ya kufungua maduka yao miezi miwli, mitatu hushangaa kuona afisa biashara anakuja  na kudai vitu kama leseni, au watu wa mamlaka ya mapato TRA wakidai TIN namba, wakati mwingine huja watu wa Halmashauri au serikali za mitaa na kudai leseni za kuuza vileo ama uwaonyesha sehemu ya wateja kujisaidia (choo) ikiwa biashara ni grosari  au mkahawa. Na wakati mwingine huja hata matapeli wajanja tu wa mjini kukutisha wakijua kabisa hukufuata taratibu za vibali ili uwape hongo ya pesa.

 

Usihatarishe biashara yako uliyoilipia pango fedha nyingi na kupoteza muda wako wa thamani, hakikisha unafuata taratibu zote hasa kupata vibali kama TIN namba, leseni kutoka ofisi ya serikali ya mtaa wako au manispaa na vibali vinginevyo ikiwa  ni biashara kwa mfano kama ya kuuza madawa ya binadamu itabidi uende mamlaka ya chakula na dawa TFDA.
0743 788 246

Jumatatu, 6 Agosti 2018

MBINU 6 ZA AU MISINGI 6 YA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA.

Ili uweze kufanikiwa, ni lazima kujiwekea misingi imara ya kimafanikio itakayokuwa ikukuongoza kila siku. Bila kuijua misingi hii mapema sitashangaa kuona maisha yako yakibaki kuwa yaleyale bila ya kubadilika sana. Kwa kujiwekea misingi hii, inauwezo wa kufanya maisha yako kubadilika kwa sehemu kubwa sana.

Kama misingi hiyo ipo, ni nini kinachokuzuia wewe kufanikiwa sasa? Bila shaka hakuna. Unachohitajika kukifanya ni kutumia misingi hiyo mpaka kufanikiwa. Uwezo na nguvu za kubadilisha maisha yako kwa kadri unavyotaka unao. Kwa kuijua misingi hii, kwako itakuwa chachu ya kukusaidia kuweza kusonga mbele na kujijengea maisha ya mafanikio makubwa:-

Je, misingi hiyo ni ipi?

Hii Ndiyo Misingi 6 Muhimu Ya Kujiwekea, Ili Kujenga Mafanikio Ya Kudumu.

Kaa mbali na watu hasi.

Kama vile ambavyo ilivyo kompyuta inaweza ikaharibiwa na virusi na kuharibika kabisa, hata wewe maisha yako yanaweza kuharibiwa vivyohivyo lakini ikiwa una watu hawa hasi wengi wanaokuzunguka. Unapokuwa na watu hasi inakuwa ni rahisi sana kwako kuweza kuua mipango na malengo mazuri uliyojiwekea.

Ninajua watu hawa wanaweza wakawa ni rafiki zako au ndugu kabisa, lakini hiyo haina namna tena kwako, zaidi ya kuachana nao. Ikiwa utaendelea kung’ang’ania kuwa na watu hawa hasi utarudishwa nyuma sana katika maisha yako. Ili kuokoa maisha yako ni lazima kukaa mbali nao na kutafuta marafiki chanya watakaokupa hamasa ya kufanikiwa zaidi. Kukaa mbali na watu hasi ni msingi mzuri kwako unaotakiwa kuujua.

Wekeza kila siku katika maisha yako.

Huu ni msingi muhimu sana kujiwekea ili kuwa na mafanikio ya viwango vya juu. Kama katika maisha yako unawekeza kila siku, tambua baada ya muda kidogo kuanzia sasa utakuwa mbali sana kimafanikio. Pengine unaweza ukaanza kusema ‘oooh mimi sasa sina pesa, sina mtaji hili halinihusu nitawekeza vipi sasa hapa?’

Sikiliza, hauhitaji kuwa na pesa ili kuwekeza. Anza na kuwekeza kwanza kwenye akili yako kwa kujifunza kupitia vitabu au semina mbalimbali. Maisha yako yatakuwa ya thamani sana kila utakavyozidi kufanya uwekezaji huu. Maarifa utakayoyapata huko kwani yataweza kukusaidia kuwekeza katika maeneo mengine na kufanikiwa zaidi pale utakapopata mtaji unaouhitaji.

Kuwa wewe kama wewe.

Kuna wakati wengi wetu huwa ni watu wa kutaka maisha ya kuwapendezesha wengine. Nikiwa na maana kutaka kuishi maisha kama wengine wanavyoishi. Hiki ni kitu hatari sana kwako kwa sababu unakuwa unaishi kwa kufuata bendera ama wengine wanavyoishi na kujikuta unakuwa mtu wa kupoteza mwelekeo.

Ili uweze kuishi kwa mafanikio ni vizuri ukajijengea msingi wa kuishi maisha yako ukiwa wewe kama wewe. Kwa kuishi wewe kama wewe itakulazimisha kutambua  unataka nini kwenye haya maisha, ni lini utafikia mipango yako uliyojiwekea na unataka kitu gani kikusaidie kufikia malengo yako. Huo ndiyo msingi muhimu pia kuujua kwa ajili ya mafanikio yako ya leo na kesho.

Jiwekee mipaka katika maisha yako.

Ishi maisha yako kwa kujiwekea mipaka. Usije ukaruhusu kila mtu kuingilia maisha yako kwa jinsi anavyotaka hata awe ndugu wa karibu kiasi gani. Bila shaka umeshawahi kuona watu ambao maisha yao yanaharibiwa kutokana na kuingiliwa na watu walio karibu nao. Na hii yote imekuwa ikitokea kutokana na wahusika kushindwa kujiwekea mipaka iliyoimara katika maisha yao.

Mipaka hii unatakiwa ujiwekee katika maeneo mabalimbali kama vile katika muda, kazi zako za kawaida na wakati mwingine kwenye biashara zako unazozifanya. Kwa kufanya hivyo watu wako wa karibu watakuwa hawako huru sana kuingilia yale maeneo uliyojiwekea mipaka maana wakifanya hivyo watajua utakuwa mkali au hutakubali kiurahisi. Hiyo itakusaidia kukujengea msingi mwingine imara wa mafanikio yako.

Kuwa king’ang’anizi wa mafanikio.

Kwenye maisha yako kitu ambacho hutakiwi kukiruhusu ni kushindwa kiurahisi. Kama ikitokea umeshindwa katika jambo kwa namna  moja au nyingne, jaribu kutafuta njia ya kulifanya jambo hilo kwa namna ya tofauti mpaka kufanikiwa. Unapokuwa king’anga’nizi wa mafanikio huo utakuwa msingi bora kwako unaojitengenezea wa kufikia mafaniko makubwa.

Maisha ni kusonga mbele. Ng’ang’ania mafanikio yako mpaka uyaone hata kwa gharama yoyote ile. Usiruhusu kitu kikakukatisha tamaa. Kama unafikira za nyuma unazoziweza kwa kudhani kuwa ulikosea eneo fulani ni bora ukaachana nazo fikra hizo kwa sasa, kwa sababu hazitakusaidi kitu chochote zaidi ya kukwamisha wewe. Yaliyopita yamepita, songa mbele.

Jijengee ukomavu wa fikra.

Ili uweze kufanikiwa inatakiwa ifike mahali fikra zako ziwe zimekomaa na kuweza kutambua kila hali inayojitokeza katika maisha na jinsi ya kuweza kukabiliana nayo. Kwa mfano, inapotokea kushindwa au ukakosea katika jambo fulani unakabiliana vipi na kushindwa huko bila kuumia au kujiona hufai na kisha kuendelea mbele.

Hakuna kingine zaidi ya wewe kuwa na ukomavu fulani wa fikra utakao kuwezesha kusonga mbele. Ukomavu huu ni rahisi kuupata, utaupata tu ikiwa wewe ni mtu wa kujifunza mambo mbalimbali ya kimafanikio kama unavyofanya sasa hivi. Bila kufanya hivyo hutaweza kuhimili mawimbi mengi ya maisha yanayojitokeza kwa upande wako.

Kumbuka hii ni sehemu ya misingi ambayo unaweza ukajiwekea kama nguzo ya mafanikio yako. Lakini, kwa kutumia kijitabu chako kidogo cha kujifunzia unaweza ukaongeza misingi mingine ambayo unaona kwako inafaa kukuongoza katika safari ya mafanikio. Bila kujiwekea misingi binafsi, utayumbishwa sana katika maisha kwa mambo mengi na itakuwa ngumu kufanikiwa.
0743788246

TIBA YA MAMBO MATANO 5 YANAYO KWAMISHA BIASHARA NCHINI

Wafanyabiashara wa Tanzania kama wale nchi nyingine,   hukumbwa na changamoto nyingi katika uendeshaji wa shughuli zao. Changamoto hizi ndizo zinaweza pia kuwa utofauti wa biashara zinazokua na zile zinazokufa.

Makala hii inachambua mambo matano ambayo huwa ni mzigo mzito kwa wajasiriamali , na pia makala inaonyesha baadhi ya njia za kukabiliana na changamoto hizo.

Kikwazo Namba 1 , Ubia:  Mara nyingi imekuwa ni ngumu kwa watu wengi kufanya biashara kwa kushirikiana na watu wengine, hususani katika hatua za mwanzo za uanzishwaji wa biashara. Vikwazo vinavyojitokeza katika kufanya ubia na watu wengine ni vingi kama vile : Kutokupata watu waaminifu, Kupata watu wasio na moyo wa kujitolea kufanya shughuli za biashara yenu, kupata watu wanaokuwa wagumu kujitolea mtaji wa kutosha kufanya biashara yenu, na zaidi sana, kupata watu wasio na muelekeo au mtazamo wa mbali wa kijasiriamali, yaani wao wanawaza faida ya haraka haraka, na kwamba kwao biashara ni sehemu ya kuingiza fedha ya ziada tuu ya leo au kesho.

Dawa yake:- Usiwe na haraka ya kufanya ubia na mtu, msome tabia yake vema. Jifunze pia kuhusu mtazamo wake wa maisha, na biashara, fahamu kuhusu familia yake na majukumu yake ya kijamii. Kisha pima uone kama majukumu yake, tabia yake, mtazamo wake , na imani yake vinaendana na biashara mnayotaka kuanzisha au malengo na mtazamo wako wa baadae wa biashara husika. Chunguza vyote kwa umakini, na usijidanganye, kumbuka dalili ya mvua ni mawingu, waweza jua mapema kama mtu atakuwa mshirika bora kwako mapema kabla hamjaanza kufanya biashara pamoja.

Usichanganye urafiki, udugu au kujuana kwa namna nyingine na biashara yako. Anaweza kweli kuwa rafiki mzuri kwako, lakini biashara yenu inahitaji mtaji wa kutosha na kujituma kwa mhusika, kitu ambacho huyo rafiki yako hatoweza kufanya kutokana  na majukumu yake ya kifamilia.

Kikwazo Namba 2, Usimamizi wa wafanyakazi: Mambo magumu yanayojitokeza katika usimamizi wa wafanyakazi ni wafanyakazi kukosa uaminifu na kuwa na ufanisi wa chini ya kiwango. Usipoangalia utapata hasara, na hata kupoteza wateja kwani wateja kwa ujumla huja kufuata bidhaa na huduma zako ambazo zinatolewa na hao wafanyakazi.

Dawa yake:- Kuna namna kadhaa za kupambana na tatizo hili. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujenga muundo mzuri wa biashara yako ikiwa pamoja na mpango bora wa kifedha ili uweze kulipa wafanyakazi kwa kiwango cha kuridhisha.

Ukishakuwa na mpango mzuri wa kifedha maana yake utaweza pia kuajiri watu wanaokidhi kiwango cha kazi unachotaka wafanye, na sio basi tuu ili mradi watu.

Kingine unachoweza kufanya ni kuweka muundo maalum wa utendaji katika biashara yako ili kila mfanyakazi afahamu majukumu yake, anaripoti kwa nani, anahitajika kufanya nini, na kwa kiwango gani. Fungua mianya ya mawasiliano ili kujua matatizo wanayokumbana nayo watendaji wako.

Zaidi sana hakikisha watendaji wanao ujuzi na vifaa vinavyoendana na kazi wafanyayo na ufanisi unaotakikana.

Tumia muda kujua tabia za watu unaotaka kuwaajiri, na endelea kuwa karibu nao na kujifunza kuhusu wao ili uweze kujua namna ya kuwachochea pia utendaji wao. Je, unafanya nini kuwachochea waonyeshe bidii na ubunifu. Je, unaruhusu ubunifu ? Je unawaheshimu na kuwathamini watendaji wako ?

Kikwazo Namba 3, Muundo wa biashara: Hili limekuwa ni tatizo kwa watu wengi hususani wafanyabiashara wadogo na wa kati. Ni tatizo zaidi kwakuwa wafanyabiashara wenyewe wengi hawaoni kama ni tatizo, wakitoa visingizio kuwa eti uendeshaji wao wa biashara ndio muundo bora zaidi  “kibongo bongo”.

Hapa nazungumzia kuwa na biashara ambayo haina mgawanyiko wa majukumu, haina mchanganuo wa biashara, haina utunzaji sahihi wa taarifa, na wala haifuati taratibu za kisheria kama usajili, kuwasilisha taarifa za fedha , kulipa kodi, kuwa na akaunti benki, n.k.

Hili ni tatizo kwa kuwa biashara hizo hazijaandaliwa kukua, na hata zinapofanikiwa kukua zinakumbana na ugumu wa kuwa endelevu.

Hivyo kuleta ugumu wa kuongeza mtaji kupitia mikopo ya benki na asasi nyingine, ugumu wa kuendeshwa kitaalamu zaidi kwani madaraka yameshikiliwa na mtu mmoja, na ugumu wa kupanua fursa za kibishara kama vile kushirikiana na biashara kubwa zaidi , kushiriki katika kuomba Tenda, n.k.

Na mbaya zaidi inapotokea mmiliki au mmoja wa wamiliki kufariki au kushindwa kuendelea kuendesha biashara, biashara huyumba na hatimaye kufa kwakuwa hakukuwa na muundo unaoeleweka wa uendeshaji wa biashara husika.

Dawa yake:-Kama haufahamu jinsi ya kuunnda muundo imara wa biashara yako,  mkodi mtu akufanyie kazi hiyo, au jifunze ili uweze kufahamu namna ya kuweka muundo vema. Heshimu taaluma za watu, na omba ushauri inapobidi.

Fanya bidii uzungukwe na wafanyakazi unaowaamini na wenye uzoefu na ujuzi wa kile wanachokifanya. Jifunze mambo mengi zaidi kuhusu usimamizi wa biashara, na kuwa macho na changamoto unazokumbana nazo kwani hizo zinakupa mafundisho ya kuboresha biashara yako.

Kikwazo Namba  4, Mtaji: Kikwazo hiki hujitokeza katika mitazamo mitatu, kwanza wakati wa kutaka kuanzisha biashara, pili wakati biashara imeshaanza ila fedha hazitoshi kuendesha vema, na tatu pale mfanyabiashara anapokusudia kupanua biashara yake.

Dawa yake: Ili kukabiliana na kikwazo cha mtaji yafuatayo yanaweza kusaidia:

Kuanza biashara kidogo kidogo: Hii namaanisha kuwa kufikiria namna ambazo unaweza kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo na wakati huo huo ukafanya kwa ufanisi. Hii inaweza kwa kuchunguza kwa umakini gharama zisizo za lazima, mambo ambayo unaweza fanya wewe mwenyewe au kusaidia na watu wengine bila kuajiri, pia chunguza aina ya bidhaa ambazo kweli ni za lazima kuanza nazo.

Kutunza taarifa za biashara yako kwa ufasaha na kuwa na muundo bora wa uongozi, hii itakusaidia kuwa kutimiza masharti ya benki, na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha ambao wanaweza kukuongezea mtaji.

Zingatia pia kuwa na mali zisizohamishika, na pia kuna na mahusiano mazuri na wadau mbalimbali kwani wao wanaweza kuwa vyanzo vya kukupatia mtaji. Mfano Badala ya kununua bidhaa kwa fedha taslimu, unaweza kukopa- mtaani tunaita “Mali Kauli”.

Kikwazo Namba 5, Ushindani wa kibiashara: Kikwazo hiki kinajitokeza kwa namna nyingi ikiwa ni pamoja na uwezekano mkubwa wa kuigwa na watu wengine. Ni kawaida watu kutaka kuiga kama ufanyavyo hasa pale unapoonekana kufanikiwa.

Kikwazo hiki hujitokeza pia katika namna ya bidhaa mpya zinazokuja kuwa mbadala wa bidhaa yako, na hata kuwa katika bei ya chini zaidi.

Kumbuka siku hizi wateja wengi wana mianya mingi ya kupata taarifa za bidhaa mbalimbali na bei zake toka kwa wauzaji mbalimbali. Hivyo kufanya biashara kwa mazoea tuu kwakuwa una ‘jina’ kubwa haitoshi.

Dawa yake:- Jifunze kusoma alama za nyakati, kwa kufuatilia habari zaidi zinazohusiana na aina ya biashara unayofanya, wafahamu wapinzani wako vema, soma taarifa pia za mambo ya kijamii, kimataifa, siasa na hata burudani, vyote hivi vinaweza kukupa muelekeo wa mambo katika jamii hivyo kujituma zaidi na wewe kubadilika.

Kujifunza kwako kuhusu wapinzani au wafanyabiashara wengine hakutokuwa na maana kama hautokuwa na muundo imara wa uendeshaji wa biashara yako, na pia ukaboresha ufanisi wako siku hadi siku.

Pia jitahidi kujenga uwezo wa kuitofautisha biashara yako na biashara nyingine , na kuwa na kitu cha kipekee ambacho wengi hawawezi kuiga, na hata kama wataiga, hawatoweza kufikia kiwango chako.

Hitimisho: Wewe msomaji kama mdau wa ujasiriamali , niambie hapa chini kwa ku comment, wadhani ni changamoto gani huwa vikwazo kwa wajasiriamali , na je tunazipatia tiba.

KUTENGENEZA SUNITAIZER

UTATENGENEZAJE SANITAIZER UKIWA NYUMBANI ILI KUJIKINGA NA CORONA Aina ya kwanza Mahitaji 🔸Vineger chupa nzima 🔸vodkta,au highlife hiz...