Nikiwa nimeketi mkononi nimeshika
kitafunwa nilichokarimiwa tayari kuanza
kula nikainua macho na kuangalia mbele
yangu na ghafla nikakutana na maandishi
kwenye kioo cha kompyuta yakihamasisha
Ongeza ufahamu kuhusu faida za kunawa mikono kwa sabuni
Maandishi hayo yakanigusa na
kunikumbusha kuwa nilipokea kile kitafunwa nikala bila kunawa mikono zaidi yakanikumbusha kuwa Oktoba 15 ilikuwa,
Siku ya Kimataifa ya Kunawa Mikono kwa Kiingereza, 'Global Handwashing Day'.
Ilinitia aibu nikaenda kutimiza kanuni ya afya kwa kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla ya kula, kisha nikaendelea na
mlo wangu huku nikiwaza na kupata
msukumo wa kuandika maelezo ili
kukumbushana umuhimu wa kunawa mikono kabla ya kula.
Sihivyotu bali pia kufanya hivyo kwa majisafi na sabuni baada ya kutoka chooni ili
kuepuka maambukzi ya vimelea vya maradhi
hatari kwa afya zetu.
Vimelea hivi huwapo kwenye mikono ambayo haikusafishwa kwa maji safi na
sabuni na huingia mwilini kila tunapokula,
Bila kunawa kwa maji safi na sabuni Siku hii hukumbukwa kila Oktoba 15 kwa
lengo la kuhamasisha kujenga kwa utamaduni wa kunawa mikono kwa sabuni,
Kwa kila taifa ulimwenguni pia kujua faida zake Kimsingi siku hiyo ilianzishwa kwa ajili ya
kuwajengea watoto na wanafunzi na watu wazima
utamaduni wa kunawa mikono,
Inaweza kuadhimishwa na mtu yeyote ndiyo maana inagusa kila jamii
kuiadhimisha kwa kila mtunikikukumbusha
wewe yule na wote manufaa na umuhimu wake katika kunawa mikono kwa maji safi na sabuni,
Takwimu zinaonyesha kuwa karibu watu 200 milioni katika nchi takriban 100 duniani hushiriki katika siku hii muhimu kiafya.
Serikali, mashirika ya kimataifa taasisi za kijamii, kampuni, mashirika yasiyo ya kiserikali na kila mmoja wetu anawajibika
pia kushiriki na kuhamasisha kunawa mikono kwa maji safi na sabuni,
Pamoja na wajibu huu unaweza kujiuliza kwa nini kunawa mikono kwa sabuni?
Kiafya kunawa mikono kwa sabuni ndiyo njia sahihi na nafuu ya kuzuia magonjwa ya
tumbo, kuhara yanayoathiri na kugharimu
maisha ya mamilioni ya watu hasa watoto katika nchi zinazoendelea kila mwaka.
Hali hiyo inamfanya kila mmoja wetu kuwajibika kwa namna moja au nyingine na vifo vya watoto wetu ambao ni taifa la
kesho, Wanaopoteza maisha kwa magonjwa yanayotokana eti na sababu ya kutonawa
mikono kwa sabuni tu.
Ni muhimu tukakumbuka jukumu muhimu katika maisha la kulinda familia zetu hasa
watoto wetu dhidi ya maradhi hata vifo
vinavyotokana na magonjwa ya uambukizo yanayowapata kwa kutonawa mikono kwa
maji safi na sabuni.
Katika hali ya kawaida, inawezekana
kunawa mikono kwa maji safi na sabuni ni zoezi gumu linalohitaji muda mrefu kujizoesha. Pia ikawa ni vigumu kuueneza
utamaduni huo wa kunawa mikono kwa
maji safi na sabuni, lakini tufanye hivyo kwa umuhimu wa kuokoa maisha ya watoto
yasipotee.
Kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla ya kula na baada ya kutoka chooni ni
utamaduni unaowezekana kujengeka
miongoni mwetu na unaweza kusaidia kwa
kiasi kikubwa kuokoa maisha yetu kuliko kinga ya dawa. Kitaalamu, Tabia hii inaelezwa kuweza kusaidia kupunguza
nusu ya vifo vinavyotokana na magonjwa ya kuhara na robo ya vifo kutokana na magonjwa ya tumbo.
Tufungue milango ya fahamu na kutambua
kwamba tukiwafundisha zaidi watoto wetu tabia hii njema ya kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla ya kula na baada ya kutoka chooni kutasaidia siyo tu kupunguza idadi ya vifo na maradhi bali tunaweza
kujenga jamii ya ustaarabu.
Maoni yako ni mhimu sana hapa chini na sisi tutayafanyia kazi tunapenda sana ushauri wako.