Jumatatu, 30 Julai 2018

MAKOSA 6 YA MATUMIZI YA PESA.

___MAKOSA KATIKA PESA__

MONEY MISTAKE 1
Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara. Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake. 

MONEY MISTAKE 2
Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako. Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo  umeahidiwa mahali fulani. Kama kuna mtu kakwambia, Flan njoo kesho nikulipe deni lako" Basi wewe usiende kukopa vitu kadhaa dukani au hata kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na wewe umeahidiwa.  Ni kosa. Unaweza kuingia kwenye matatizo.

MONEY MISTAKES 3
Kama unataka kuhifadhi/kutunza pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza kiasi kitakachosalia. Hivyo basi,  ukipata tu pesa,  weka pembeni kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi kilichobaki. 

MONEY MISTAKE 4
Ukipata nafasi ya kuonana na mtu tajiri, kamwe usiombe pesa.  Omba maarifa ya kutengeneza pesa kama yeye, tena kwa mtaji mdogo.  Maarifa ndio mtaji wa kwanza.  Unaweza kupewa/kusaidiwa pesa iwapo una mawazo mazuri ya kuzalisha pesa. Baadhi husema,  "Omba ndoano, usiombe samaki"

MONEY MISTAKE 5
Usitunze mbegu badala ya kuipanda.  Watu wengi hufurahia pesa wanayolipwa/kuipata  kisha wanaiweka bank au nyumbani bila kuiwekeza. Wekeza pesa ili uzalishe zaidi.  Usiogope kuingia hasara, kila aliefanikiwa alipoteza kwanza kabla hajafanikiwa. Wengi walipoteza muda, pesa, afya na hata matumaini ya kufanikiwa, ila kwa uthubutu wao, mwisho wa siku walifanikiwa.

MONEY MISTAKE 6
Kamwe usimkopeshe mtu pesa ambayo unahisi hatorudisha.  Unapomkopesha mtu huyo pesa,  jiridhishe mwenyewe moyoni kuwa kama hatoweza kulipa basi deni lake halitoathiri urafiki wenu. Ukihisi kwamba kushindwa kwake kulipa kunaweza kuathiri urafiki wenu, basi mshauri aende bank akakope.

MONEY MISTAKE 7
Usikubali uwe shahidi , tena kwa kusaini kabisa ili umdhamini mtu ambae huna uhakika kuwa atalipa kile unachomdhamini. Kumbuka kuwa,  dhamana maana yake utawajibika iwapo atashindwa kulipa.

MONEY MISTAKE 8
Epuka kutembea na pesa nyingi ambazo hata huna matumizi nazo wakati huo. Unaweza kujikuta unafanya matumizi ambayo hayakuwa kwenye ratiba sababu ya ushawishi wa pesa ya mfukoni. Ili kuepuka haya,  tembea na pesa uliyopanga kuitumia katika safari yako. Pesa nyingine itunze mahali pengine palipo salama. 

MONEY MISTAKE 9
Epuka kutunza pesa mahali pasipo sahihi.  Maeneo kama kwenye soksi,  sidiria,  chini ya mto wa kulalia,  chini ya begi,  kwenye kopo au hata kwenye begi la safari, si maeneo salama.  Ni rahisi kusahau,  kuibiwa au kupoteza pesa zako.  Ni bora ukatunza pesa kieletroniki; yaani bank au kwenye simu au kwenye pochi yenye kamba ngumu ya kuivaa mabegani au wallet ambayo inatosha kwenye mifuko imara na yenye vifungo kwenye nguo zako hasa uwapo safarini. 

MONEY MISTAKE 10
Usitumie pesa kwa kitu ambacho hakikuwa kwenye ratiba yako. Jiulize kwanza kabla hujanunua, "Bila kitu hiki, maisha yataenda au lah? Ukiona maisha yataenda bila kitu hicho, acha kukinunua. Tabasamu kisha ondoka.

MONEY MISTAKE 11
Usiingiwe tamaa kwa kununua kitu ambacho ungeweza kununua kwa bei ya punguzo mahali pengine zaidi. Labda tu uwe una pesa nyingi.

MONEY MISTAKE 12
Matumizi yako ya pesa yasizidi pato lako. Unaweza kuwa una ndoto kubwa/matumizi makubwa ya pesa kuzidi pato lako.  Unapaswa kuwa bahili katika matumizi yako. Cheza na pato lako.  Fanya matumizi makubwa pale tu pato lako litakapoongezeka.  Hii itakuepushia kushindwa kufanya baadhi ya mambo ya msingi na kisha ukajikuta unaishia kwenye madeni makubwa. 

💰MONEY MISTAKE 13
Una ndoto kubwa hapo baadae; labda kujenga nyumba,  kununua gari,  kununua kiwanja, simu nzuri hata pikipiki. Usikurupuke,  ukanunua kitu cha ndoto yako sasa eti tu sababu umekipata kwa bei ya punguzo. Usichanganye kati ya mahitaji ya baadae na ya sasa. Pesa unayotumia kutimizia ndoto sasa itumie kwa mahitaji ya sasa. Ndoto ibaki kuwa ndoto. Hii itakuepushia kuingia katika madeni au kuishi kwa shida sababu ya tamaa. Jipange taratibu kutimiza ndoto yako.

Jumatano, 18 Julai 2018

Abiola Solidarity Group: Karibu solidarity

Abiola Solidarity Group: Karibu solidarity: Karibu solidarity hiki kikundi cha wajasiriamali kina jishughulisha na utangenezaji wa sabuni aina zote, Kila mtanzani anahaki ya kujiunga ...

Jumanne, 17 Julai 2018

FUNGUA MACHO NA FIKRA.

FUNGUA MACHO NA FIKRA ZETU KWA PAMOJA

KITU AMBACHO WENGI HAWAKIFAHAMU NI KUWA MAKAMPUNI MAKUBWA YOTE YA BINAFSI NI MJUMUIKO WA WATU WENGI WALIOUNGANISHA PESA ZAO, UTAALAM WAO NA KUJITOA KWAO KUTENGENEZA KAMPUNI HIZO HATA KM JINA LINALOVUMA NI LA MTU MMOJA KTK KAMPUNI HIYO, KIWANDA HICHO

HATA VIWANDA VYA SERIKALI VINGI NI MJUMUIKO WA SERIKALI NA UBIA EIDHA WATU WA NDANI AU MATAIFA MENGINE YA KUTOKA NJE

HIVYO BASI SOLIDARITY IMEDHAMIRIA KUUNGANISHA NGUVU ZA WATU WA CHINI NA WAKATI KUANZISHA KIWANDA CHA USINDIKAJI KWA MTAJI MDOGO KWA LEO MKUBWA HAPO SIKU ZIJAZO WAKATI WALIOTHUBUTU WAKIENDELEA NA WALIODHARAU WAKIHITAJI NAFASI KUJIUNGA NA INUKA

USICHOKIJUA TUU NI KUWA: MTU KM MOHAMED, REGINALD ,SAID NA HATA HUYU MTENGENEZA KARANGA KWA SASA WOTE HAO NYUMA YAO WANAMISURURU YA WATU WALIOUNGANA KTK KUWEKEZA KTK LILE TUNALOLIONA MACHONI PETU

TUSIJIDHARAU HATA SISI SOLIDARITY TUKIWEKA NIA,DHAMIRA,UTHUBUTU TUTAFANYA MASIKIO YA WATU TZ NA NJE YA TZ KUTUSIKIA KILA SIKU TUKIKATA MAWIMBI KTK VYOMBO TOFAUTI VYA HABARI TUKIZALISHA BIDHAA TOFAUTI ZA VYAKULA NA VINYWAJI

TUSIMAME IMARA SASA kwani TZ YA VIWANDA HATA KWA SISI HUMU INAWEZEKANA

Jumatatu, 16 Julai 2018

MISINGI MITANO 5 MHIMU YA KUFANIKIWA KWENYE UJASIRIAMALI NA BIASHARA

Misingi Mitano 5 Muhimu Ya Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali na Biashara.

Katika ulimwengu wa sasa ambao ajira zimekuwa ngumu na shida kupatikana, ujasiriamali na biashara vimekuwa ndio kimbilio la wengi. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kama njia kuu ya kujipatia kipato.

Pamoja na biashara kuonekana kuwa kimbilio la wengi sio wote wanaoingia kwenye biashara wanafanikiwa. Tafiti zinaonesha kwamba asilimia tisini ya biashara zinazoanzishwa zinakufa mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Na hata hizo zinazovuka mwaka mmoja asilimia tisini hufa baada ya miaka mitano. Hivyo kama mwaka huu zimeazishwa biashara mia moja basi miaka mitano ijayo ni biashara moja tu itakayokuwa bado inadumu.

Kwa nini biashara nyingi zinashindwa kudumu?

Biashara nyingi zinakufa kutokana na ukosefu wa elimu muhimu kuhusiana na biashara na ujasiriamali. Watu wengi wanaoingia kwenye biashara wanaingia kwa kuangalia tu ni kitu gani watu wengine wanafanya na wao kufanya hivyo hivyo.

Biashara ni rahisi sana kufanya ila ni ngumu kuendesha na kuikuza mpaka iweze kukupa faida kubwa sana. Ili uweze kuendesha na kukuza biashara itakayokupa faida kubwa ni muhimu kuchukua muda na kujifunza vitu vya muhimu vinavyohusiana na biashara.

Leo tutajifunza misingi mitano muhimu ya biashara ambayo kila biashara inatakiwa kuizingatia. Wewe kama mjasiriamali una jukumu la kujifunza na kufuata misingi hii ili uweze kufikia malengo yako kwenye ujasiriamali na biashara.

Misingi mitano muhimu ya biashara.

Ili biashara yoyote iweze kudumu na kukua inahitaji kufuata misingi ifuatayo.

Kutengeneza thamani.

Ili biashara iweze kukua na kutengeneza faida ni lazima itengeneze bidhaa au huduma ambayo ni ya thamani kwa wateja. Ni lazima utoe bidhaa au huduma ambayo watu wanaihitaji sana ili kuboresha maisha yao. Kama hujaanza biashara fikiria ni kitu gani cha thamani ambacho watu wanakihitaji ila wanakikosa, kisha anza kuwapatia na utajenga biashara kubwa. Kama tayari unafanya biashara angalia ni kitu gani cha thamani unachotoa kwa watu na angalia jinsi unavyoweza kuboresha ili kupata wateja wengi zaidi.

Soko.

Kuwa na kitu chenye thamani pekee bado haikutoshi kutengeneza biashara kubwa, ni lazima kuwe na soko linalohitaji bidhaa au huduma hiyo. Hata kama soko lipo bado sio rahisi kwa kila mtu kujua kwamba unatoa huduma muhimu. Hivyo ni muhimu kutafuta soko la biashara yako kwa njia mbalimbali zikiwemo matangazo. Inakubidi uhakikishe watu wanajua uwepo wa biashara yako na utengeneze uteja ili watu waje kupata thamani unayotoa. Kukosa soko la uhakika ni chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.

Kuuza.

Ili biashara ikue ni lazima uweze kuuza thamani uliyotengeneza. Ni muhimu uweze kuwashawishi watu wanunue bidhaa au huduma unayotoa. Kuuza ndio moyo wa biashara ambapo kama usipokuwa makini ni rahisi kwa biashara kufa.

Kufikisha thamani.

Kama umewaahidi wateja wako kwamba bidhaa ama huduma unayotoa itaboresha maisha yao basi hakikisha hicho ndio kitu kitakachotokea kwa wateja. Ni lazima uweze kufikisha thamani uliyoahidi kwa wateja. Kwa kushindwa kufanya hivi wateja watakuona wewe ni tapeli na hawatanunua tena bidhaa yako. Kama biashara itashindwa kutengeneza wateja wanaojirudia ni lazima itakufa.

Fedha.

Usimamizi wa fedha ni muhimu sana kwenye biashara. Ili biashara iweze kudumu ni lazima iweze kutengeneza mapato makubwa kuliko matumizi na uzalishaji. Ni lazima iweze kuzalisha fedha za kutosha kuiendesha na ibaki faida. Ukosefu wa fedha unaotokana na mauzo kidogo na matumizi makubwa ndio chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.

Misingi hii mitano ni muhimu sana kwa biashara. Hakuna msingi ambao unaweza kusema ni muhimu zaidi ya mwingine, yote inategemeana. Ili biashara yoyote iweze kudumu ni muhimu kuzingatia misingi hiyo. Endelea kutembelea blog yetu ili uweze kupata makala mengi ya yenye faida kwako au tupigie
0762 291 395
0743 788 246
Usikubali kushindwa kirahisi penda kushinda wakati wote usisahau kumuomba Mungu.

Ijumaa, 13 Julai 2018

KUTENGENEZA MSHUMAA

Mishumaa ni bidhaa mojawapo ambayo ni bidhaa nzuri Na itumikayo kila Siku katika maisha yetu ya kila Siku kwa maana zina matumizi ya kutuletea mwanga pia hutumika kanisani Na sehemu zingine mbalimbali .

Utengenezaji WA mishumaa .

Malighafi au nahitaji muhimu

1;paraffin wax
2:utambi
3:hardener
4:mould au umbo
5:stearine
6:boric acid
7:sufuria
8;chanzo cha moto
9:rangi
10:citronella
11:perfume

Miongoni mwa malighafi hizo si zote utatumia Bali kuna malighafi hizi Kama rangi .citronella Na perfume hizi malighafi si lazma kutumika ila ni nzuri kwa ajili ya kuboresha bidhaa yako.

Matumiz ya malighafi hizi

1:citronella  Hii ni malighafi ambayo husaidia kuua wadudu sehemu ulipo hii hasa hutumia kwa ajili ya Kutengenezea mishumaa ya kuua mbu

2:rangi 
Hii ni kwa ajili ya kuboresha muonekano Wa bidhaa yako .
Pia rangi zitumikazo ni rangi za vyakulaa

3:perfume
Hii pia ni malighafi ambayo huleta harufu katika bidhaa yako

4:hardener 
Hii hufanya kazi ya kuganfisha mishumaa

5;boric acid
Hii ni dawa kwa ajili ya kulowekea utambii
Pia inasaidia mishumaa usitoe moshi kwa maana unafanya carbon iishie kwenye utambi

6:stearine
Hii kufanya mshumaa uwake muda mrefu

7:bee wax 
Hilo nu hitaji muhimu katika utengenezaji Wa bidhaa hii ambapo hili kutokana Na masega ya nyuki pia huchanganywa Na mafuta ya petrol au diesel pia rangi Yake ni njano

8:paraffin wax 
Hii ni hitaji kubwa Sana katika utengenezaji WA mishumaa hii ni zako LA nyuki linaloyokana Na Nta Pamoja Na masega ya nyuki ambapo huchanganywa Na mafuta ya taa.
Rangi yake ni nyeupe
Pia paraffin wax ni nzuri zaid Kutengeneza mishumaa kuliko bee wax
9: mould 
Haya ni maumbo mbalimbali ya mishumaa ambayo Kutengenezea pia unachagua umbo Gan utumie yako ya round Na ya pembe Na design mbalimbali ya mould
Uwiano Wa malighafi

1: stearine vijiko 3vya chakula

2:paraffin wax au bee wax kilo Moja
3:hardener vijiko viwili Vya chakula
4:boric acid weka kulingana Na wingi Wa tambi zako
5:rangi citronella Na perfume weka kidogo kidogo

Weka kwa ueiano huo kadri unavyoongeza am a kupunguza kiasi

Zingatia kuwa kuvaa gloves ni muhimu kila unapozalisha mishumaa yako.
Powered by @abiola_solidarity_group

UTARATIBU WA KUJIUNGA NA SOLIDARITY

UTARATIBU WA KUJIUNGA NA SOLIDARITY
Unatakiwa kutoa kiasi cha Tsh laki moja na nusu tsh150,000/= Kwa mchanganuo kama ifuatavyo tsh 30,000 ni pesa ya dharula endapo mwanachama atapatwa na matatizo yasiyo zuilika kikundi kitatoa pesa hii ya dharula kuna kiwango kimepangwa kwa manachana kama unaungaulia nk tsh120,000/=

KIKUNDI KINA OFFICE YAKE
Kila mwanachana mpya ambaye anahitaji kujiunga na solidarity inakupasa ulipie kiasi cha Tsh30,000 kwa maana hii kwamba utakuwa umelipia gaharama za uendeshaji wa office yako ya solidarity

KIASI CHA TSH 100,000 LAKI MOJA
Hii pesa ndiyo kiingilio mahususi unatakiwa kulipa kwa mwanachama mpya ambayo itakufanya kuwa mwanachama mpya na hai ukisha kujiunga utakuwa kama mwanchama mwanzilishi wa kikundi siku ikifika ya kupapa gawio la kikundi na wewe mwanachama ulie ingia leo upata gawio hilo kama mwanachama wa zamani au mwanzilishi

UNUNUAJI WA HISA
Mwanachama ukishajiunga unatakuwa kuwa unanunua hisa kwa sababu tayari umesha kuwa mmiliki wa hiki kikundi Kikundi hakiwezi kusonga mbele bila kuwa na fedha pia wanachana wanatakiwa kuzalisha pesa zao zile wanaziweka kwenye kikundi hicho hivyo basi unapaswa kununua hisa kila siku hisa moja unauzwa kwa tsh2000 kila mwanachama anatakiwa kununua hisa 3 kila wiki moja

FAIDA YA KUNUNUA HISA
Kila mwanacha anawekeza pesa yake ifanye kazi kwahiyo unaponunua hisa utapata mkopo kwenye kikundi chako ambapo utapata mkopo wa riba nafuu sana tena wenye 5%_10% kwa mkopo huu hua hauna mashart hata kidogo maana wewe ni mmiliki wa kikundi hiki

Kama hujaelewa vizuri basi usisite kutupigia au kuwasiliana nasi via .abiolasolidaritygroup@gmail.com
simu no:_ 0743 788 246
                  0673 835 098
Karibu sana solidarity ni kiwanda

Karibu solidarity

Karibu solidarity hiki kikundi cha wajasiriamali kina jishughulisha na utangenezaji wa sabuni aina zote,
Kila mtanzani anahaki ya kujiunga na kikundi hiki masharti ya kujiunga na kikundi hiki ni kuanzia umri wa miaka 18 nk,
Malengo ya kikundi hiki ni kuwa na kiwanda cha kikundi hapo baadae je kikundi kinapata je pesa ya kujenga kiwanda?
Nikwamba kikundi mbali na utengenezaji wa sabuni pia tunatengeneza batiki,ufundishaji wa ujasiriamali na ununuaji wa hisa na kuuza hisa kwa kila mwanacha wa kikundi hiki pia kutoka mtu wa nje,
Tunatoa mkiopo ili kuweza kupata pesa kukuza mtaji wa kuweza kununua mashine za utengenezaji wa sabuni nk mkopo unatolewa kwa mwanachama hai na mtu wa nje asie mwanachana
mbali zaidi tunafundisha mtu mmoja mmoja na vijundi mbali mbali tunatoa elimu ya ujasiriamali kwa wanakina mama na vijana wote pamoja wakina Baba pia kama unapenda kujiunga na kikundi hiki sasa usisite kujiunga karibu sana tupigie na tuandikie 0743788146 au kwenye email yetu abiolasolidaritygroup@gmail.com njoo tulijenge taifa letu pamoja na maisha yetu.

KUTENGENEZA SUNITAIZER

UTATENGENEZAJE SANITAIZER UKIWA NYUMBANI ILI KUJIKINGA NA CORONA Aina ya kwanza Mahitaji 🔸Vineger chupa nzima 🔸vodkta,au highlife hiz...