Jumanne, 25 Septemba 2018

UMHIMU WA KUNUNUA HISA NA FAIDA ZAKE.

FAIDA NA UMHIMU WA KUNUNUA HISA

Wajasiriamali wanashauriwa kusoma baadhi ya vitabu ambavyo waandishi wameandika mada mbalimbali za ujasiriamali ikiwamo uwekezaji katika hisa.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 84 ya Watanzania wakiwamo wasomi na wengine ambao hawajabahatika kusoma hawajui au hawana elimu kuhusu kuwekeza katika hisa.

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba mada hii haijawekwa katika mitaala mbalimbali ya elimu. Kama ipo basi wale wanaostahili kuifundisha ama hawana uelewa mpana na uzoefu wa kuwawezesha wanafunzi wao kufahamu umuhimu wake katika medani za kiuchumi.

Hisa inaelezeka kwa namna mbalimbali, kwa ujumla wake hisa ni mali, rasilimali, kitegauchumi, hati miliki, biashara, dhamana ya mkopo, ni akiba, ni fedha iliyohifadhiwa, na ni mtaji.

Katika mtazamo wa kibiashara, hisa ni uwekezaji wa mtaji au fedha ambayo imewekezwa na mfanyakazi, mkulima, mfanyabiashara au mtu mwingine ambaye ameamua kununua hisa kutoka katika kampuni fulani kwa lengo la kupata faida kupitia gawio na ongezeko la bei ya hisa husika.

Uwekezaji katika hisa kama biashara nyingine unahitaji umakini na upembuzi yakinifu. Kufanya upembuzi wa wapi uwekeze fedha zako na wapi ununue hisa kwa msingi wa kupata faida.

Mjasiriamali au watu wengine wanaweza kufanya upembuzi yakinifu, lakini kama watu makundi niliyoyataja hapo juu wana uelewa wa kutosha na mbinu za kusoma taarifa mbalimbali za kampuni ambayo unakusudia kununua hisa. Kwa mfano, unapaswa kufanya upepenuzi yakinifu wa taarifa za fedha na hali halisi ya kampuni husika
katika soko la hisa.

Kwa upande mwingine, washauri wataalam wana ujuzi wa kufanya upembuzi yakinifu katika masuala ya uwekezaji kwenye soko la mitaji ambao wa wanapatikana kwenye masoko ya hisa katika jengo la Habour-view, mtaa wa Samora, jijini Dar es Salaam.
Ununuzi wa hisa unaweza kufanywa katika soko la awali mathalani pale kampuni inapotangaza kuuza hisa zake.
Baada ya kampuni kutangaza kuuza hisa, watu wananunua kwa thamani halisi, lakini baadaye zinauzwa katika soko la hisa ambako thamani ya hisa inabadilika kuendana na hali ya soko.

Tukiangalia upande wa kampuni, mpaka Agosti, mwaka huu kulikuwa na zaidi ya kampuni 16 zilizosajiliwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE). Kampuni 11 ni za kizalendo na kampuni sita ni za nje.

Kwa mujibu wa Emilian (2010), asilimia 0.39 tu ya Watanzania wamewekeza kwenye soko la hisa. Kutokana na tatizo hilo, bado ni tatizo kubwa kwa Watanzania na kwa jicho la pili ni fursa kubwa kwa wajasiriamali, wafanyakazi na wanafunzi kuwekeza katika hisa.

Uwekezaji katika hisa unachangamoto zake ikiwzmo kushuka kwa bei ya hisa, kukosa gawio, mfumuko wa bei, viwango vya riba, kukosa wanunuzi kutokana na ukwasi na hitilafu mbalimbali.

Kwa hali ya kawaida uwekezaji katika hisa una faida nyingi kuliko changamoto kwa mfano, kupata gawio baada ya kampuni kutengeneza faida, ongezeko la thamani ya hisa, punguzo la kodi ya zuio kwenye gawio.

Katika masuala ya hisa, hakuna kodi kwenye ongezeko la thamani, urahisi wa kuuza na kununua hisa, na ukiwekeza katika hisa unapata muda wa kufanya shughuli nyingine. Kwa upande mwingine hisa ni dhamana ya kupata mkopo, hisa ni urithi mzuri, ukijiwekea utaratibu wa kutenga asilimia fulani ya pato lako kutoka kwenye mshahara ama biashara kwa ajili ya kununua hisa ni uamuzi mzuri, na hisa pia ni utajiri

Tuna kukaribisha kuanza sasa kununua hisa katika soko la hisa katika kikundi cha @ABIOLA_SOLIDARITY GROUP Utapata faida kubwa katika kuwekeza hisa zako huwezi kujutia ndg mtanzania

Wasiliana nasi no
              0743 788 246
              0759 408 410
              0762 291 395
abiolasolidaritygroup@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUTENGENEZA SUNITAIZER

UTATENGENEZAJE SANITAIZER UKIWA NYUMBANI ILI KUJIKINGA NA CORONA Aina ya kwanza Mahitaji 🔸Vineger chupa nzima 🔸vodkta,au highlife hiz...